Ad Code

Responsive Advertisement

NAMNA YA KUCHEZA KARATAELIMU


KarataElimu ni kwa kila mtu, awe mwanafunzi, mzazi, mlezi au mwalimu. Kwa mfano, wanafunzi wanaweza kucheza kadi hizi kwa ajili ya kujifunza wenyewe. Wazazi au walezi wanaweza kucheza kadi hizi pamoja na watoto wao. Walimu pia wanaweza kuzitumia kadi hizi kucheza na wanafunzi wao au kuwaongoza wanafunzi kucheza ili kujifunza vizuri Kiingereza. Kwa ujumla, KarataElimu hizi ni mchezo wa kuburudisha na kujifunza pia. 

Kuna namna moja ya kucheza hizi kadi. Lakini malengo ya uchezaji ndio yanaweza kuwa tofauti pamoja na ‘level’ au umri wa mwanafunzi. Kwa ujumla, hizi kadi zinahusisha kucheza na kujifunza kwa pamoja. Mchezo huu wa kadi huchezwa kama kadi za kawaida ambazo tunazifahamu. Tofauti na zile tulizozizoea, hizi ni kwa ajili ya kujifunza tu japo na kuburudika ndani yake. Pamoja na kwamba, kadi hizi ni kwa ajili ya kujifunza Kiingereza, lakini huchezwa kwa Kiswahili. Japo kama wacheza watakubaliana au watakuwa wameumudu mchezo, wanaweza kutumia Kiingereza wanapocheza. 

AINA ZA KARATAELIMU

Kadi za KarataElimu ziko za aina tatu: 

1) KarataElimu za Misamiati 



Mada: Nomino (Nouns)

Idadi ya Kadi: 56

Idadi ya Maneno: 280 (Nomino zote za msingi za Kiingereza)   

Idadi ya Misamiati (Nomino zate za msingi za Kiingereza): 275 

Ujuzi lengwa: maana, tahajia (spelling), matamshi (pronunciation and reading), na matumizi (usage). 

Wanafunzi lengwa: Wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari pamoja na Watu Wazima.  


2) KarataElimu za Misamiati



Mada: Vitenzi (Verbs

Idadi ya Kadi: 56

Idadi ya Maneno: 280 (Vitenzi vyote muhimu vya Kiingereza)  

Idadi ya Misamiati (Vitenzi vyote muhimu vya Kiingereza): 275 

Ujuzi lengwa: maana, tahajia (spelling), matamshi (pronunciation and reading), na matumizi (usage). 

Wanafunzi lengwa: Wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari pamoja na Watu Wazima.


3) KarataElimu za Kujifunza Kuzungumza Kiingereza kwa njia ya maswali



Mada: Kuzungumza Kiingereza (Kupitia maswali)

Idadi ya Kadi: 36

Idadi ya Maswali: 144 (Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara katika kuzungumza Kiingereza) 

Ujuzi lengwa: kuzungumza na kusoma (speaking and reading) 

Wanafunzi lengwa: Wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari pamoja na Watu Wazima.


FAIDA ZA KARATA ELIMU

KarataElimu hizi zinamsaidia mwanfunzi kujifunza yafuatayo: 

(1) Kujiamini kuzungumza Kiingereza, 

(2) Kuongea/kutamka Kiingereza, 

(3) Kusikiliza Kiingereza, 

(4) Kusoma Kiingereza. 

(5) Kuandika Kiingereza, na 

(6) Kuweza kuwasiliana kwa Kiingereza katika mazingira mbalimbali. 


HATUA ZA KUCHEZA KADI ZA KIINGEREZA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI PAMOJA NA SEKONDARI PIA

HATUA ZA KUCHEZA KARATA ZA MISAMIATI (NOUNS & VERBS): Kila kadi ina maneno matano. 

Zifuatazo ni hatua za kucheza KarataElimu za maswali: 

(1) KUWA NA WACHEZAJI ZAIDI YA MMOJA. 


(2) KUWA NA MWALIMU AU MTAALAM WA LUGHA (Grammarian). Huyu kazi yake ni kuwaongoza wachezaji endapo watashindwa kabisa kutoa maana ya neno au kuwapa msaada wowote kabla, wakati, na baada ya mchezo. Kama Mwalimu au ‘Grammarian’ atalazimika kutoa maana ya neno ambalo wachezaji wote wameshindwa kujibu, basi Mchezaji aliyetaja neno husika atacheza ile karata kama kawaida lakini hatahesabiwa kama amepata goli au Kombe. 


(3) KUCHANGA NA KUGAWA KARATA: Changa na gawa karata kama kawaida. Mara nyingi huwa ni kadi 3 au 4 kwa kila mchezaji. 


(4) HAKUNA KADI YA KUANZA MCHEZO: Usiweke kadi ya kuanza mchezo.


(5) MCHEZAJI WA 1: Anayeanza mchezo anasoma neno mojawapo alilochagua kati ya matano yaliyo kwenye kadi mojawapo. (Huyu anajifunza kusoma/kutamka Kiingereza)


(6) MCHEZAJI WA 2: Mchezaji wa 2 anatakiwa kutaja maana ya neno. Akishindwa anatakiwa kulamba/kuokota kadi/karata nyigine. (Huyu anajifunza kusikiliza na kutoa maana kwa Kiswahili). Akiweza kutoa maana, anaruhusiwa kucheza kadi yoyote kati ya zile alizonazo. 


(7) MCHEZAJI WA 3, 4, 5 n.k: Kama mchezo unahusisha wachezaji hadi watano n.k, wachezaji hawa nao wanatakiwa kutaja maana ya neno lililotajwa na Mchezaji wa 1 (au mchezaji yeyote). Nao wakishindwa wanatakiwa kulamba/kuokota kadi/karata nyigine. Na mmoja wao akiweza kutoa maana, anaruhusiwa kucheza kadi yoyote kati ya zile alizonazo. 


(8) KUTOA MAANA YA NENO: Mchezaji atakayefanikiwa kutaja maana ya neno, anatakiwa kucheza kadi yoyote kati ya zile alizokuwa nazo na inakuwa zamu yake kucheza kwa kutaja neno lolote kutoka kwenye kadi mojawapo ili wenzake wataje maana yake. 


(9) MCHEZAJI WA 1: Kama wachezaji wote wameshindwa kutoa maana, Mchezaji wa 1 (au mchezaji yeyote) aliyetaja neno anatakiwa kutoa maana ya neno. Akiweza kutoa maana sahihi, acheze karata yake yenye neno alililotaja awali. Akishindwa kutoa maana sahihi, hatakiwi kucheza na anatakiwa kulamba karata. 


(10) MCHEZAJI 2, 3, 4, 5 n.k akipata/akipatia maana sahihi ya neno, anatakiwa kucheza karata yoyote kati ya zile alizonazo na hatakiwi kulamba/kuokota kadi, na inakuwa ni zamu yake kucheza kwa kutaja neno ili wenzake watoe maana yake.


(11) MSHINDI: Mchezaji anayemaliza kadi mkononi ndio anakuwa mshindi wa mchezo kisha karata zinachangwa kwa ajili ya mchezo mpya. 


(12) MTOANO: Wachezaji wanaweza kuamua kuwa kila baada ya mchezo mmoja kumalizika, mchezaji mwenye karata nyingi mkononi anapaswa kutolewa kwenye mchezo au wanaweza kuachana na mtoano na wote wakacheza hadi mwisho. Mchezo unaweza kufika hadi fainali ambayo itakuwa na wachezaji wawili na baada ya fainali mchezo utaanza upya. Idadi ya magoli (goli 1 kwa mchezo mmoja) itahesabiwa na anayeshinda fainali anakuwa ameshinda Kikombe. Katika mazingira ya shule, Mwalimu anaweza kuandaa zawadi kwa kila goli (mchezo) na kila Kombe. 


NB: Baada ya wachezaji kucheza mara kadhaa, utaratibu wa kutaja/kutamka maneno yote matano ya kwenye kadi unaweza kutumika pia. Badala ya kutaja neno moja na kutoa maana, wachezaji hutaja maneno yote ya kwenye karata na wenzake kutakiwa kutoa maana kwa kila neno. Anayepatia kutoa maana ya maneno yote anakuwa ameshinda, na utaratibu mwingine wa mchezo unaendelea kama kawaida (kama Hatua 1 hadi 12 hapo juu).


Pia wachezaji wanaweza kwenda mbali zaidi. Ambapo mchezaji akitaja neno wengine wanapaswa kutunga sentensi ya Kiingereza kwa kutumia neno lililotajwa.


HATUA ZA KUCHEZA KARATA ZA MASWALI (COMMUNICATIVE APPROACH): Kila karata ina maswali matano. 

Zifuatazo ni hatua za kucheza KarataElimu za maswali: 

(1) KUWA NA WACHEZAJI ZAIDI YA MMOJA. 


(2) KUWA NA MWALIMU AU MTAALAM WA LUGHA (Grammarian). Huyu kazi yake ni kuwaongoza wachezaji endapo watashindwa kabisa kujibu swali au kuwapa msaada wowote kabla, wakati, na baada ya mchezo. Kama Mwalimu au ‘Grammarian’ atalazimika kutoa jibu sahihi kwa swali ambalo wachezaji wote wameshindwa kujibu, basi Mchezaji aliyeuliza swali husika atacheza ile karata kama kawaida lakini hatahesabiwa kama amepata goli au Kombe. 


(3) KUCHANGA NA KUGAWA KARATA: Changa na gawa kadi kama kawaida. Mara nyingi huwa ni kadi 3 au 4 kwa kila mchezaji. 


(4) HAKUNA KARATA YA MCHEZO: Usiweka karata ya kuanza mchezo. 


(5) MCHEZAJI 1: Anasoma swali mojawapo kutoka karata aliyoichagua. 


(6) MCHEZAJI WA 2: Mchezaji wa 2 anatakiwa kujibu swali kwa Kiingereza. Akishindwa anatakiwa kulamba/kuokota kadi/karata nyigine. (Huyu anajifunza kuongea na kusikiliza). Akiweza kutoa maana, anaruhusiwa kucheza karata yoyote kati ya zile alizonazo. 


(7) WACHEZAJI WOTE, yaani 2, 3, 4, 5 n.k wanatakiwa kujibu swali kwa Kiingereza. Kwa mfano: Mchezaji A: Where do you live? Mchezaji B: I live at Mtakuja Village (Asijibu kwa ufupi kama vile ‘At Mtakuja Village’). Wakishindwa wanatakiwa kulamba/kuokota kadi/karata nyigine. 


(8) MSHINDI: Mchezaji yeyote kati ya 2, 3, 4, 5 n.k akijibu swali vizuri, atacheza karata yake yoyote na atauliza swali moja kutoka kwenye karata mojawapo kati ya alizobaki nazo. 


(9) MCHEZAJI 1: Kama wachezaji wote kati ya 2, 3, 4, 5 n.k watashindwa kujibu swali, Mchezaji 1 ( au mchezaji yeyote) aliyeuliza anatakiwa kujibu swali kwa usahihi – na yeye akishindwa kujibu kwa usahihi anatakiwa kulamba karata. 


(10) MCHEZAJI YEYOTE KATI YA 2, 3, 4, 5 n.k akijibu swali kwa usahihi atacheza karata yoyote aliyonayo na hatakiwi kulamba karata. 


(11) MSHINDI: Mchezaji anayemaliza kadi mkononi ndio anakuwa mshindi wa mchezo kisha karata zinachangwa kwa ajili ya mchezo mpya. 


(12) MTOANO: Wachezaji wanaweza kuamua kuwa kila baada ya mchezo mmoja kumalizika, mchezaji mwenye karata nyingi mkononi anapaswa kutolewa kwenye mchezo au wanaweza kuachana na mtoano na wote wakacheza hadi mwisho. Mchezo unaweza kufika hadi fainali ambayo itakuwa na wachezaji wawili na baada ya fainali mchezo utaanza upya. Idadi ya magoli (goli 1 kwa mchezo mmoja) itahesabiwa na anayeshinda fainali anakuwa ameshinda Kikombe. Katika mazingira ya shule, Mwalimu anaweza kuandaa zawadi kwa kila goli (mchezo) na kila Kombe. 



NB: Baada ya wachezaji kucheza mara kadhaa, utaratibu wa kutaja/kutamka maneno yote matano ya kwenye kadi unaweza kutumika pia. Badala ya kutaja neno moja na kutoa maana, wachezaji hutaja maneno yote ya kwenye karata na wenzake kutakiwa kutoa maana kwa kila neno. Anayepatia kutoa maana ya maneno yote anakuwa ameshinda, na utaratibu mwingine wa mchezo unaendelea kama kawaida (kama Hatua 1 hadi 12 hapo juu).


Hitimisho

Ili kupata matokeo mazuri ya KarataElimu, ratiba na usimamizi mzuri vinahitajika sana. Mfano; wachezaji wanaweza kucheza kila siku au baada ya siku 2 au 3. Lakini msimamizi ambaye ni Mwalimu, mzazi au mlezi anatakiwa kufuatilia ili kuona kama wanafunzi wanajua maana ya maneno yote na wanaweza kujibu maswali kwa Kiingereza na kwa ufasaha. 



ZAIDI:

Tembelea Kachele Online Blog


Download vitabu HAPA!


Jipatie maswali na majibu (BUREE!) HAPA!


Jipatie KITABU CHA MASWALI YA KIINGEREZA ZAIDI YA 5,000 NA MAJIBU YAKE HAPA!


Jipatie KITABU CHA KUJIFUNZA KIINGEREZA CHA KUZUNGUMZA (MASOMO 60) HAPA!

 

Post a Comment

0 Comments

Close Menu